Pichani nikiwa na mjasiriamali wa kazi za mikono kutoka Dar. Waoneshaji wamelalamikia kukosa watembeleaji kwenye mabanda yao. Maonesho haya yanafanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri,Morogoro. Yanatajiwa kumalizika hapo kesho.
Hapa nikiwa napata maelezo kuhusu mashine ya kuyeyusha shaba
Wadau wa Greenhead wakikabidhi mpira kwa waalimu mara baada ya mechi.
Pichani ni wadau wa Greenhead college kutoka Uk,na CHINACO wakiwa kwenye jezi ya Taifa star kabla ya kukipiga na timu ya waalimu wa shule ya msingi kinole.
Pichani kushoto ni mwenyekiti wa mtaa wa choma bi Zinduna Kombo na kulia mwenyekiti wa Chilunga Nature Conservator's(CHINACO) ndugu Godwill Herbert akimkabidhi kivukio. CHINACO kupitia programme yake ya chilunga cultural tourism ilishirikiana na mtaa wa choma katika kutekeleza mradi huo.
Pichani ni mandhari ya soko la Morogoro japo ni la zamani twapata mahitaji yetu.On photo is appearance of Morogoro central Market although is old,it satisfies our needs.
Karibu uje ujionee yote haya kwenye Fahari Afrika cultural Event hapo tarehe 25/09/2009 ndani ya mji kasoro bahari.You are welcome to see all these,in Fahari Afrika Cultural Event on 25/09/2009 in Morogoro.
Teknologia huanzia huku.Hawa ni waundaji wa magari wa siku zijazo kama wakiendelezwa.Here is where technology starts.On photo are future car manufacturers.
kama ilivyokawaida ndani ya FACE mwezi huu ni msondo ngoma "Baba ya muziki" ni tarehe 25/09/2009 ndani ya Tush club na 26/09/2009 usisite kujiandikisha kwa ajili ya kupanda mlima."kama miguu yako haijafika, macho yako hayajaona"
Pichani ni watalii wa kuangalia ndege.On photo are bird watchers
Kila siku Jumamosi CHINACO wakishirikiana na WCST huandaa utalii wa kuangalia ndege.Jumamosi waanzia Rock garden hadi ofisi za mali asili kuanzia saa moja asubuhi.
Every saturday CHINACO in collaborations with WCST organize bird watching.This week tour will start from rock garden to regional natural&tourism office at 7:00 am.
Pichani ni mwenyekiti wa mtaa wa choma na kamati ya ujenzi wa kivuko,wakiwa na wadau wa CHINACO baada ya kikao cha makualiano ya ushirikishwaji katika ujenzi.CHINACO kupitia Chilunga cultural tourism programme wanashirikiana na wanachoma katika ujenzi huo.
Hili ni kaburi la anasadikiwa ndie mwazilishi wa mji wa Morogoro Chifu Kingo kisabengo.Kaburi limetelekezwa,kama likituzwa linaweza kuwa kivutio cha utalii.